Michuano ya kombe
la mabara itaendelea tena leo hii kwa michezo miwili ya kundi A
kuchezwa, wenyeji Urusi watashuka katika dimba la Otkrytiye Mjini
Moscow, kucheza na Ureno .
Na mchezo wa pili wawakilishi wa bara la Afrika katika michuano hiyo timu ya Cameroon watashuka katika dimba la Fisht Olympic kupepetana na New Zealand , mchezo huo utachezeshwa na mwamuzi Bakary Gassama kutoka Gambia.
Urusi ndio vinara wa kundi A wakiwa na alama tatu baada ya kupata ushindi dhidi ya New Zealand, Ureno na Cameroon wao wana alama moja moja na New Zealand wanaburuza mkia wakiwa hawana alama hata moja.
0 comments :
Post a Comment