Hifadhi
ya taifa ya Serengeti, yenye ukubwa wa kilometa za mraba 14,763, ni hifadhi ya
pili kwa ukubwa nchini ( baada ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha).
Serengeti
ni moja kati ya hifadhi maarufu sana duniani. Umaarufu wa hifadhi hii unatokana
na misafara mirefu ya nyumbu wanao hama kwa makundi makubwa kutoka upande mmoja
wa mbuga hadi mwingine, na kuvuka mpaka wa Tanzania hadi hifadhi ya taifa ya
maasai mara nchini Kenya. Wakichagizwa na mvua kila mwaka zaidi ya nyumbu
milioni moja, pundamilia 200,000, swala 300,000 huunga misafara ya kutafuta
malisho na maji. Uhamaji huu umeipataia sifa ya kuwa moja ya maajabu saba ya
asili ya Afrika.
Hifadhi
ya Serengeti pia ni maarufuu kwa wanyama walao nyama kama chui na simba. Ukubwa
wa hifadhi hii umesaidia sana kudumisha uhai wa wanyama walio katika hatari ya
kutoweka kama faru weusi na duma. Uwapo Serengeti utashuhudia wawindaji kama
duma wanavyowinda, aidha zipo aina mbalimbali zaidi ya 500 za ndege.
Leo
kwa ufupi, tutakupatia mambo kumi (10) kuhusu Hifadhi ya Serengeti ambayo
ungependa kuyajua na kusimilua kwa wenzanko ambao hawakupata kuyajua;
1. Mfumo wa Mazingira wa hifadhi ya
taifa Serengeti ni kongwe katika dunia. Hifadhi hii inatunza viumbe hai
mbalimbali ikiwemo mimea na wanyama ambavyo vingine havipatikani mahali popote
duniani.
|
Mfumi wa uhamaji wa Nyumbu wa Serengeti |
2. Serengeti
ni nyumba ya moja ya maajabu ya asili saba ya dunia. Zaidi ya nyumbu
milioni moja uhama kwa kuvuka mto Mara na kuelekea hifadhi ya taifa ya
Maasai Mara kwa upande wa Kenya katika kutafuta malisho yao. Na hukaa
Kenya kwa mwezi mmoja tu na miezi iliyobaki hutumia mda wao wakiwa
Tanzania
|
Misururu ya nyumbu wakihama kutoka upande mmoja kwenda mwingine katika hifadhi ya Serengeti |
3. Katika
miaka zaidi ya milioni moja iliyopita, hifadhi ya Serengeti imebaki
kuwa ya asili kwa kiasi kikubwa bila kuathiriwa na mabadiliko ya
kimazingira. Wanyama pori, mimea na mikondo ya maji bado kwa kiasi
kikubwa ni ya asili kama ilikuwa miaka milioni moja iliyopita. Kwa
kushangaza, mabaki ya zamani ya mtu (miaka milioni 2 iliyopita)
yaligunduliwa hapa na mtu maarufu Afrika Mashariki archaeologist, Dr.
Leakey.
|
Binadamu wa kale aliepata kuishi maeneo ya serengeti miaka milion 2 iliyopita |
4.
Watalii wengi huvutiwa na Hifadhi hii na kushuhudia zaidi ya nyumbu
milioni moja wakiwa wanahama kwa kufatilia malisho yao. Hata hivyo,
punda milia pia huhama pamoja na nyumbu, angalau kwa idadi ndogo.
|
Pundamila pia huama pamoja na nyumbu katika hifadhi ya Serengeti |
5. Maelfu
ya wanyama wanaohama wengine hushindwa kukamilisha safari yao kutokana
na kuliwa na mamba na wanyama wengine walao nyama.
|
Nyumbu wakivuka moja ya mito inayopatikana Serengeti |
6. Serengeti
National Park inapatika kati ya futi 3020 na futi 6,070 juu ya usawa wa
bahari. Hali ya hewa yake kwa ujumla ni kavu lakini inapata mvua nyingi
katika miezi ya Juni na Julai
|
Kipindi cha mvua Serengeti |
7. Serengeti
kwa kiasi kikubwa ni ya uoto wa savannah na vichaka vilivyotawanyika na
ambavyo ni bora kwa ajili ya wanyama walao nyasi na nzuri kwa ajili ya
wanyama walao nyama pia. Miongoni mwa wanyama wapatikanao hapa ni pamoja
na, pundamilia, tembo, twiga, nyumbu, swala , paa na nyati. Miongoni
mwa wanyama walao nyama wanaopatikana ni pamoja na simba, duma , chui,
fisi , mbweha, nk
8. Serengeti
ni chimbuko la jamii maarufu ya Wamasai kabla ya kuhamishiwa katika
maeneo ya mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro mnamo mwaka 1959.
Wamasai ni moja ya jumuiya za Kiafrika kwamba ambazo bado huishi kwa
kuzingatia mila zao za kale na utamaduni kama vile tohara , ngoma na
kafara.
|
Wamasai wakiwinda na silaha za jadi |
9. Eneo
la Hifadhi ya Ngorongoro awali lilikuwa sehemu ya hifadhi ya serengeti
mpaka 1951 wakati Uingereza walipolitenga kwa ajili ya utafiti kama
binadamu na wanyamapori wanaweza kuishi pamoja katika sehemu moja bila
ya kuathirana.
10. Kwa
mara ya kwanza utafiti wa kina juu ya mazingira ya Serengeti ulifanywa
na raia wawili wa Ujerumani ( baba na mwana ) , Dk Bernhard na Michael
Grizmek . Maelezo ya matokeo ya tafiti za Serengeti ziliwekwa na
kuhifadhiwa kama kumbukumbu katika kitabu chao maarufu kinachoitwa “Serengeti shall never die.”
|
Dr. Bernard Grizmek na mwanae Michael Grizmek wakiwa katika tafiti zao kwenye Hifadhi ya Serengeti. |
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments :
Post a Comment