NDEGE YA KIJESHI YA URUSI YAITISHIA ILE YA MAREKANI BALTIC

Ndege ya Urusi ilipaa futi tano juu ya ndege ya ujasusi ya Marekani katika anga ya bahari ya Baltic siku ya Jumatatu, kulingana na maafisa wa Marekani.
Ndege ya Marekani ya ujasusi aina ya US RC-135

Hatua hiyo ilionekana kuwa isio salama kutokana na kasi ya ndege hizo mbali na udhibiti mbaya wa ndege hiyo, maafisa hao walisema.

Lakini Urusi imepinga malalamishi hayo ya Urusi ikisema kuwa ndege hiyo ya Marekani iliichokoza ndege yake.Siku ya Jumatatu Urusi iliionya Marekani kwamba ndege za Marekani zinazopaa juu ya ngaa ya Syria zitalengwa.tangazo hilo lilijiri ili kujibu kuangushwa kwa ndege ya Syria baada ya kulenga waasi wanaoungwa mkono na Marekani.

Siku ya Jumanne, Jeshi la Marekani liliiangusha ndege isiokuwa na rubani inayomilikiwa na Iran nchini Syria na hivyobasi kuongeza wasiwasi kati ya Washington na Moscow ambayo ni mshirika mkuu wa utawala wa Syria.
 Ndege ya Ursui aina ya Su-27 ilipaa futi tano juu ya ndege ya Marekani
Uchokozi huo wa siku ya Jumatatu ulifanyika kilomita 40 kutoka eneo la Urusi la Kalinigrad katika maji ya kimataifa.

Msemaji wa Pentagon Nahodha Jeff David aliambia maripota kwamba:Tulikuwa tukipaa katika maji ya kimataifa na hatukufanya uchokozi wowote.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment