Mkuu wa kundi
linalofuatilia utekelezwaji wa mkataba wa amani nchini Sudan Kusini
amesema kwa sasa hawawezi kumkubali makamu wa rais mpya aliyeapishwa
kuchukua pahala pa Dkt Riek Machar.
Festus Mogae, ambaye ni rais
wa zamani wa Botswana, ameambia BBC kwamba uchunguzi unafaa kufanywa
kubaini iwapo maafisa waliomteua Taban Deng Gai, walikuwa na mamlaka ya
kufanya hivyo.Bw Deng Gai aliteuliwa na kundi ambalo limekuwa likimpinga Dkt Machar katika mrengo wake wa SPLM
Machar, ambaye aliteuliwa makamu wa kwanza wa rais kama sehemu ya mkataba wa amani kati ya upande wake na Rais Salva Kiir, amepinga kufutwa kazi kwake.
Bw Mogae ameshutumu kile alichosema ni uhasama baina ya wanasiasa nchini Sudan Kusini jambo ambalo anasema limesababisha maafa kwa raia.
Amesema hali nchini Sudan Kusini imeendelea kuwa mbaya, na amesisitiza kwamba kikosi cha kulinda amani cha kanda kinafaa kutumwa nchini humo.
0 comments :
Post a Comment