Mtandao wa kijamii wa Facebook umetoa tamko kwamba unataka kujitenga na mazingira ya uhasama kwa watu wanaoweka maudhui tata ama watu wenye viashiria ama matendo ya kigaidi. Kauli hii imekuja baada ya Waziri mkuu wa Uingereza , Theresa May, kuzitaka kampuni zinazojihusisha na masuala ya teknolojia kuchukua juhudi za makusudi kukabiliana na maudhui yenye mrengo wa kigaidi.
Kufuatia kauli hiyo , Facebook imetamka kwamba kuanzia sasa itakuwa ikiondoa mara moja, maudhui yenye viashiria vya ugaidi.
Mtandao wa Twitter wao wamejinasibu kwamba kazi hiyo yakuondoa ama kufutilia mbali maudhui tatanishi na kamba mwaka wa jana pekee ulifanikiwa kuondoa maudhui ya aina hiyo kutoka katika akaunti elfu nne na kwamba ulijiongeza katika matumizi ya teknolojia .
0 comments :
Post a Comment