Kamati ya Bunge la Seneti la masuala ya usalama nchini Marekani imechapisha ushahidi utakaotolewa na mkurugenzi aliyetimuliwa kazi FBI ambaye amesema Rais Trump alimtaka mkurugenzi huyo kuacha kumchunguza mshauri wa zamani wa masuala ya usalama.
Wakili wa Trump amesema rais Trump anahisi kuna ukweli kwa uthibitisho kuwa yeye mwenyewe binafsi hakuwa akichunguzwa kwa timu yake ya kampeni zake kuhusishwa na Urusi.
Maafisa wawili wanaohusika na usalama,Mike Rogers na Dan Coats wamewaambia maseneta kuwa hawakuwahi kulazimishwa kufanya jambo lolote ambalo liko kinyume na sheria.
Hii ni moja ya majopo pamoja na idara ya sheria, kuchunguza ripoti za mashirika ya ujasusi ya Marekani kuwa wadukuzi wa Urusi waliingilia kati uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba.
Pia kuna uchunguzi kuhusu ikiwa kundi la kampeni ya Trump lilishirikiana na wadukuzi wa Urusi madai ambayo Urusi inayakanusha.
0 comments :
Post a Comment