FIGO ATAKA RONALDO ARUHUSIWE
MKONGWE Luis Figo amezisikia taarifa za Real Madrid kumng’ang’ania Cristiano Ronaldo na alichokifanya ni kuiambia klabu yake hiyo ya zamani kuachana naye.
Kwa mujibu wa Figo, Madrid hawatakiwi kupagawa, kwani hakuna mchezaji ambaye pengo lake halizibiki.
Ronaldo amekuwa akihusishwa na mpango wa kuondoka Madrid na hiyo imetokana na kashfa ya ukwepaji kodi inayomwandama.
“Naaamini hakuna pengo lisilozibika, si Cristiano Ronaldo pekee,” alisema Figo.
“Klabu haiwezi kumtegemea yeyote. Historia ya klabu hizi iko juu ya mtu yeyote, hata rais au mtu mwingine.”
Baada ya Ronaldo kudai kuwa anataka kuondoka, klabu yake ya zamani ya Manchester United imekuwa ikimfuatilia na hata matajiri wa Ufaransa, PSG wamekuwa wakimhitaji.
0 comments :
Post a Comment