PARIS, Ufaransa
WINGA wa zamani wa Manchester United, Angel di Maria, ameingia kwenye
kashfa ya ukwepaji kodi na tayari amekubali kulipa kitita cha Pauni
milioni 1.76 ili kumaliza kesi hiyo.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi Hispania, Muargentina huyo alifanya uhuni huo alipokuwa akiichezea Real Madrid.
Mchezaji huyo wa PSG kwa sasa, alitajwa kutolipa kodi katika mapato yake ya haki za picha akiwa na mabingwa hao wa La Liga.
Inaelezwa kuwa, hakulipa kitita cha Euro milioni 1.3 katika msimu wa 2012-2013.
Kama si kutenda kosa hilo kwa mara ya kwanza, sheria za Hispania zingemtaka Di Maria kutumikia kifungo cha miezi nane gerezani.
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment