ZANZIBAR YAKARIBIA KUWA MWANACHAMA WA FIFA.


Rais wa shirikisho la kandada nchini Tanzania (TFF) Jamal Malinzi, amethibitisha juhudi mpya za Zanzibar kuwa mwanachama wa Fifa.



Image result for picha ya timu ya taifa ya zanzibar

  Zanzibar, ambayo kirasmi ni sehemu ya Tanzania lakini iliyo na serikali yake, ilipata idhini rasmi na shirikisho la CAF mwezi Machi.

Visiwa vya Zanzibar vimekuwa na matumaini ya muda mrefu kuwa mwanachama wa shirikisho la kandanda la kimataifa na maombi yake ya awali yalikataliwa na Fifa mwaka 2005.

Shirikisho la kandanda visiwani Zanzibar (ZFA) tayari limetimiza mahitaji muhimu kwa kuwa mashirika ya kitaifa, lazima yawe wanachama wa yale ya bara kabla ya kujiunga na Fifa.

Ikiwa Fifa itakubali mwanachama huyo wa 55 wa Caf, basi visiwa vya Zanzibar vitakuwa mwanachama wa 212 wa shirikisho hilo la kandanda duniani.

Atakuwa na haki ya kupiga kura kuamua masuala ya kimataifa ya kandanda na kikosi chake kitakuwa na fursa ya kushiriki mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment