Staa wa zamani wa soka wa taifa la England na vilabu
vikubwa barani ulaya man united na real Madrid, DAVID BECKHAM amezua gumzo hivi
karibuni mara baada ya kuonekana kwenye hifadhi ya Serengeti iliyopo nchini
Tanzania.
BECKHAM aliingia kwa siri nchini akionekana kuja na
familia yake kwa ajili ya mapumziko mara baada ya ligi tofauti tofauti barani
ulaya kumalizika.
Hata hivyo beckham hakusita kuonyesha hisia zake kwa
real Madrid mara baada ya kutazama mpira akiwa kwenye ardhi ya Tanzania na
kuweza kuipongeza timu hiyo ambayo aliitumikia kwa muda kabla ya kwenda
kumaliza soka lake nchini marekani.



0 comments :
Post a Comment