Rais wa Marekani Donald Trump
ameutaja utawala wa taifa la Korea Kaskazini kuwa wa kikatili kufuatia
kifo cha mwanafunzi mmoja wa Marekani ambaye alikuwa amefungwa jela kwa
zaidi ya miezi 15 nchini humo.
Bwana Warmbier ambaye alifungwa kwa kujaribu kuiba bango la propaganda kutoka kwa hoteli moja hakuweza kupata fahamu tena.
Bwana Trump alisema kuwa kifo cha Warmbier kimeimarisha mipango ya utawala wake wa kutaka kuwatetea wengine kupata majanga kama hayo katika mikono ya mataifa yasioheshimu sheria.
''Marekani kwa mara nyengine inashutumu ukatili wa utawala wa Korea kaskazini huku tukimkumbuka mwathiriwa wa hivi karibuni''.
Wazazi wa Warmbier Fred na Cindy walisema katika taarifa kwamba mwanao alifariki siku ya Jumatatu katika hospitali ya Cincinnati ambapo alikuwa akipewa matibabu.
Wanasema kwamba wakati Otto aliporudi Cincinnati alikuwa hawezi kuzungumza na hakuweza kuona.
0 comments :
Post a Comment