Wakizungumza katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam wiki hii, Madereva wameihitaji Sumatra kuweka vipengele na sheria zitakazotofautisha makosa yao na ya wamiliki, ili kila mmoja awajibike katika nafasi yake pale inapotakikana.
Aidha, madereva wa bodaboda pia wameeleza kero za tozo kubwa za faini kwa makosa mbali mbali na kupaza sauti zao wakiihitaji Sumatra kuangalia swala hili la faini kubwa dhidi yao ili kuwatengenezea mazingira ya unafuu katika kufanya shughuli zao za kila siku, hususani wakati huu ambapo biashara ya bodaboda imekuwa ngumu ukilinganisha na siku za nyuma. Rasimu hiyo inatarajiwa kujadiliwa na kufikia maamuzi kabla haijaidhinishwa na waziri wa wizara husika
0 comments :
Post a Comment