Shirikisho la soka duniani Fifa
limetetea mfumo mpya wa teknolojia ya Video uliobuniwa kuwasaidia Marefa
kutoa maamuzi sahihi (VAR) kuwa teknolojia hiyo itafaa sana katika
mchezo wa mpira wa miguu siku za mbeleni.
Lengo shirikisho hilo la
soka ni kuona teknolojia hiyo inatumika katika fainali za michuano ya
kombe la dunia ya mwaka 2018 ambazo pia zitachezwa Nchini Russia.
Rais
wa Fifa Gianni Infantino amesema : "Tumeona namna teknolojia hii ya
video inavyoweza kuwasaidia waamuzi kufanya maamuzi sahihi uwanjani.
Katika
maelezo ya Fifa katika matukio matano yaliyotokea kwenye michuano ya
kombe la mabara yakaamuliwa na teknolojia hiyo imeonyesha manne ni ya
kuzidi na moja ni la mchezaji kushika mpira.
Gianni Infantino anataka Majaribio ya VAR yafanikiwe
ili teknoloji hiyo ipitishwe kuweza kutumika rasmi katika fainali
zijazo za kombe la dunia.
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment