Nyota wa muziki wa Pop nchini Marekani Beyonce amejifungua mapacha kulingana na vyombo vya habari nchini Marekani.
Beyonce ambaye ni mkewe mwanamuziki wa mtindo wa Rap Jay Z alitangaza kwamba ni mjamzito katika picha ya Istangram mnamo mwezi Februari ambapo ni picha iliopendwa mno katika historia ya mtandao huo.
Wawili hao tayari wana mwana wa kike, kwa jina Blue Ivy aliye na umri wa miaka mitano.
Hakujakuwa na tangazo rasmi kuhusu kujifungua huko kutoka kwa Beyonce na Jay Z mwenyewe.
Picha nyengine zilizochapishwa na Beyonce baada ya kutangaza kuwa ni mjamzito ziliomuonyesha akiogelea chini ya maji, akiwa katika maua huku akiwa amekaa uchi ndani shada la maua.
Katika picha moja mwimbaji huyo wa wimbo 'Lemonade' alisimama akiwa uchi na kushikilia tumbo lake na mkono mmoja na mwengine akishikilia titi lake , mbele ya kichwa cha kiongozi wa zamani wa Msiri.
0 comments :
Post a Comment