BARAKA THE PRINCE ATAJA SABABU ZA KUTOKUWA NA ALIKIBA KARIBU


Moja kati ya story ambayo iliwahi kuchukua headlines nyingi katika mitandao siku za nyuma ni kuhusu staa wa Bongofleva Baraka the prince kutokuwa karibu na staa mwingine Alikiba baada ya kuwa pamoja wakifanya shuguli za muziki.


Baraka the Price amefunguka na kueleza sababu za watu hao kutokuwa karibu tangu alipotoa wimbo aliomshirikisha Alikiba akisema sababu ni kuwa buys akiandaa album yake mpya.

Akiongea kwenye XXL ya Clouds FM Baraka the Prince amedai kuandaa albamu yake mpya kumemfanya awe busy huku Alikiba akiwa kwenye tour nje ya nchi: 

Ujue mimi natoa Albam mwaka huu kwa hiyo tangu mwaka umeanza nimekuwa busy natengeneza album yangu ndio maana sionekani niko karibu na Ali. Kwanza Ali amekuwa haonekani Dar es Salaam sana. Amekuwa yupo safarini na tunakuwa tunawasiliana sana kwenye simu na massage lakini ile kuonekana kama zamani ni kwa kuwa yupo kwenye kazi zake na mimi nipo kwenye kazi zangu.

“Zamani kilichokuwa kinatufanya tuwe karibu ni kwa sababu tulikuwa tufanya kazi ya kutukutanisha. Tulikuwa chini ya Rock Star kampuni moja na ikitokea suala la wasanii wa Rock Star lazima utaniona niko na Ali lakini sasa hivi nilikuwa na maandalizi ya album yangu na inakaribia kwisha.” – Baraka the Prince
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment